MHE.RAHMA KASSIM ALI  AMEFANYA ZIARA  KATIKA MAHAKAMA YA ARDHI
21 Mar 2022

MHE.RAHMA KASSIM ALI AMEFANYA ZIARA KATIKA MAHAKAMA YA ARDHI Featured

  

WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Rahma Kassim Ali amewasisitiza watendaji wa Mahakama ya ardhi kuhakikisha wanatenda haki wakati wanapotoa maamuzi ya kesi za migogoro ya ardhi zinazowasilishwa mahakamani hapo.

Akizungumza na watendaji hao huko katika ofisi za mahakama ya ardhi Mwanakwerekwe katika ziara yake ya kuangalia utendaji kazi wa mahakama hiyo Mhe. Rahma alisema kua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeunda  chombo hicho kwa lengo la kusimamia haki za wananchi na kuondosha  migogoro ya ardhi nchini ambayo imekua ikirudisha nyuma jitihada za kuleta maendeleo.

Mhe. Rahma Kaasim Ali akisema kua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeunda  chombo chombo cha Mhakama ya Ardhi

kwa lengo la kusimamia haki za wananchi na kuondosha  migogoro ya ardhi nchini 

 

“Serikiali imeunda chombo hichi kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi kwa kesi zinazowasilishwa hapa hivyo watendaji wanapaswa kutenda haki na kutoa maamuzi sahihi bila ya kumdhulumu mtu yoyote”alisema Mhe Rahama.

Aidha alifahamisha kua ardhi ni kitu muhimu kwa vile Taasisi  hiyo ipo katika kuhudumia jamii ni vyema kwa watendaji wa mahakama kuhakikisha wanatatua kesi kwa haki na usawa na kila mwenye haki yake apewe mwenyewe kwa muda stahiki kwa mujibu wa sheria na kanuni za kimahakama na si jambo la busara kuona kua kesi zinachukua muda mrefu katika kupatiwa ufumbuzi wake.

“Ningeliomba mwenendo wa kesi uende kwa haraka kwa mujibu wa sheria na tuhakikishe hazichukui muda mrefu katika kupatiwa ufumbuzi wake kwani kinyume na hapo unamkosesha mwananchi kufanya mambo yake ya kimsingi kwa kutumia muda mwingi kusibiria kesi ipatiwe ufumbuzi”alisisitiza Mhe.Waziri.

Sambamba na hayo Mhe. Rahma aliwataka watendaji hao kua na utaratibu wa ufatiliaji wa kesi hizo mara tu zinapowasilishwa mahakamani hapo kabla ya kutoa maamuzi sahihi.

“Kabla ya kutoa maamuzi tuwe na utaratibu wa ufatiliaji ili kuepusha kutoa haki kwa asie husika na kupelekea kuibuka kwa migogoro mengine ndani yake”alisema Mhe Rahma.

Hata hivyo Mhe.Rahma aliwataka watendaji hao kutojihusisha na upokeaji wa rushwa katika utendaji wa kazi za kimahakama sambamba na kujitahidi kudhibiti siri za Chombo hicho huku wakitambua kua wamebeba zamana kubwa ya kulitumikia Taifa kwa maslahi ya nchi na wananchi wake.

“Si jambo jema kuona mtendaji anapokea rushwa katika utoaji wa huduma kwa jamii huku akitambua kua kitendo hicho ni kinyume na utaratibu wa majukumu yake ya kazi hivyo”alisisitiza.

Hata hivyo aliwataka watendaji hao  kua wabunifu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ili kuweza kulipatia sifa taasisi tunazozitumikia na kupiga hatua Zaidi ya kimaendeleo na kiuchumi.

Ni vyema kwa watendaji kua wabunifu katika kubuni vitu vyenye kuleta faida kwa jamii pamoja na kuisadia Serikali hasa katika masuala ya ardhi.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mahakama ya ardhi Mwanakwerekwe Khamis Rashid Khamis alifahamisha kua  Serikali ilipitisha sheria namb.1 moja ya mahakama ya ardhi mwaka 1994 ambapo mwaka 2008 Serikali pia ikaona ipo haja yakufanya marekebisho ya sheria nomb.7  ya Mahakama ya ardhi na kuanzisha mahakama ya ardhi kwa kila mikoa ya Unguja na Pemba kwa lengo la kusogeza huduma hiyo karibu na  jamii na kuondoa migogoro ya ardhi nchini ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.

 

Mwenyekiti wa mahakama ya ardhi Mwanakwerekwe Khamis Rashid Khamis alifahamisha kua  Serikali ilipitisha sheria nomb.1

moja ya mahakama ya ardhi mwaka 1994 ambapo mwaka 2008 Serikali pia ikaona ipo haja yakufanya marekebisho ya sheria namb.7  

ya Mahakama ya ardhi na kuanzisha mahakama ya ardhi

Nao wafanyakazi hao wameahidi kuyafanyia kazi yale yote aliyowaelekeza na kuiomba wizara kuangalia uwezekano wa kupatiwa eneo kwa ajili ya utanuzi wa ofisi kwani jengo wanalolitumia ni dogo na halikidhi mahitaji jambo linalokosesha ufanisi mzuri wa kazi sambamba na kupatiwa mafunzo yanayoendana na kazi zao pamoja posho maalum kwa wafanyakazi wa kitengo cha utunzaji siri za kimahakama.