Mhe. Waziri wa Ardhi na Naibu Waziri wamefanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Kamisheni ya Ardhi
14 Mar 2022

Mhe. Waziri wa Ardhi na Naibu Waziri wamefanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Kamisheni ya Ardhi

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Rahma Kassim Ali amewataka watendaji wa Kamisheni ya Ardhi kuhakikisha wanafanyakazi kwa mujibu wa Sheria na miongozi ya kiutumishi ili kuweza kuleta ufanisi kazini.

Akizungumza katika ziara yake ya kwanza ya kuitembelea Taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara yake Mhe Rahma alisema kua  Kamisheni ya Ardhi ni taasisi muhimu katika utoaji wa huduma kwa jamii hivyo nivyema kwa watendaji hao  kufuata sheria na miongozo ya kiutumishi ili kwenda sambamba na kasi ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika taasisi tunazozitumikia.

Alifahamisha kua mfanyakazi yoyote anatakiwa ajitathmini yeye mwenyewe binafsi kwa kiasi gani anawajibika katika majukumu yake  na si jambo la busara kua kila mara awe anafatiliwa na kusimamiwa jambo ambalo linapelekea kutokua na ufanisi mzuri katika kazi na kurudisha nyuma juhudi za kiutendaji.

Mhe.Rahma Kassim Ali amewataka watendaji wa Kamisheni ya Ardhi kuhakikisha wanafanyakazi

kwa mujibu wa Sheria na miongozi ya kiutumishi ili kuweza kuleta ufanisi kazini.

Aidha Mhe Rahma ameitaka taasisi hiyo kuhakikisha inaboresha mazingira yake kwani mazingira yalioko sasa hayaendani na hali halisi ya kiutendaji.

Hata hivyo Mhe.Rahma aliwataka pia watendaji hao kua waadilifu na waaminifu hasa katika kitengo cha manunuzi ambacho ndio msimamiizi wa matumizi na mahitaji ya kiofisi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Nadir Abdullatif Yussuf amesisitiza haja kwa watendaji hao kuwa wabunifu katika kazi jambo ambalo litapelekea kuipatia hadhi taasisi hiyo na kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Mhe.Nadir amewahakikishia watendaji hao kua mbali na changamoto wanazokabiliana nazo kuendelea kua

wazalendo katika kulitumikia taifa na changamoto hizo atazifanyia kazi kadri hali itakavyoruhusu.

Alifahamisha kua kuna baadhi ya watendaji hawako makini katika majukumu hivyo kuacha tabia hiyo nakutekeleza majukumu yao kama walivyopangiwa na wakuu wao wa kazi.

Hata hivyo Mhe.Nadir amewahakikishia watendaji hao kua mbali na changamoto wanazokabiliana nazo kuendelea kua wazalendo katika kulitumikia taifa na changamoto hizo atazifanyia kazi kadri hali itakavyoruhusu.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Kamisheni ya Ardhi Sleiman Haji Hassan alimelezea Mhe Waziri kua kwa sasa wamejitahidi kuweka mazingira mazuri  ya kiutendaji na kuhakikisha kila mfanyakazi anawajibika ipasavyo katika utekelezaji wa kazi zake za kila siku.

Katibu Mtendaji Kamisheni ya Ardhi Sleiman Haji Hassan akimuelezea Mhe Waziri kua kwa sasa wamejitahidi kuweka

mazingira mazuri  ya kiutendaji na kuhakikisha kila mfanyakazi anawajibika ipasavyo katika

utekelezaji wa kazi zake za kila siku.

Ziara ya Mhe.Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Kazi ni akiwa ameambataa na viongozi wa Wizara hiyo ikiwa na lengo la kuzitambua taasisi zake na kuangalia namna wanavyoendesha shughuli zao za kiuetendaji za kila siku.