WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI YAPOKEA VIFAA VYA KOMPYUTA

 MSAADA WA KOMPYUTA

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imepokea  jumla kompyuta destop 4 na Printer 4 za rangi kutoka kwa Kampuni ya Milele foundation kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kazi.

 

Akizungumza mara ya kupokea msaada huo huko ofisini kwake Maisara Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Riziki Pembe Juma amesema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka na vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa.

 

Aidha Mhe.Pembe ameushukuru uongozi mzima wa Milele Foundation kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunafikia malengo ya kuleta maendeleo katika nchi kupitia taasisi mbalimbali.

 

Kwa upande wake muakilishi kutoka milele Foundation  Mudrik Said Suleiman alisema kua kutokana umuhimu wa Taasisi hiyo wameona ipo haja ya kushirikiana nao katika kuwapatia vifaa ili viweze kuboresha kasi ya utendaji.

 

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi 12  million vimetolewa taasisi ya milele foundation na kukabidhiwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi .