KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI IKIPOKEA RIPOTI YA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI
25 Nov 2021

KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI IKIPOKEA RIPOTI YA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI

KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI IKIPOKEA RIPOTI YA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI

 

KAMATI ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi, imeipongeza Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kupitia Shirika la Nyumba la Zanzibar kwa kufikia asilimia 291 ya makadirio ya makusanyo yake katika kipindi cha Julai –September 2021.

 

 

kikao cha majumuisho ya kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi na viongozi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi , kilichofanyika katika Wizarani Maisara

 

Akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya kamati na viongozi wa wizara hiyo, kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo Maisara, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ali Sleiman Ameir, alieeleza kuwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa Wizara kupitia Shirika lake la nyumba kwa kipindi hicho inaridhisha.

 

 

Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Ali Sleiman Ameir, akieeleza kuwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa Wizara kupitia Shirika lake la nyumba kwa kipindi hicho inaridhisha.

 

 

Hata hivyo mwenyekiti huyo alisema kuwa Shirika la nyumba halina budi kusimamia ipasavyo majukumu yake kufanya hivyo kutapelekea kupatia sifa Wizara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unakwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya nchi yetu.

 

“Tunalipongeza shirika la nyumba kwa usimamizi mzuri katika vyanzo vyake vya mapato hakikisheni manongeza bidi na maarifa ili shirika liweze kupiga hatua zaidi’’ alisisitiza.

Aidha Mwenyeki huyo wa Kamati ya Bajeti amezitaka taasisi nyengine zilizo chini ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuiga mfano mzuri ulioneshwa na Shirika la Nyumba ili kuweza kufikia malengo waliyojipangia na kuiongezea mapato Serikali.

“tunaziomba taasisi nyengine zilizo chini ya Wizara ya Ardhi kuiga Mfano mzuri waliounesha Shirika la Nyumba katika jitihada za kutekeleza majukumu yake kwa bidi na kuhakikisha mapato yake yanaongezeka alisema”

 

Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo ametoa pongezi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuja na mradi wa ujenzi wa nyumba za viongozi ambao unasimamiwa na Wizara ya Ardhi kwa lengo la kuboresha makaazi bora na kuweka muonekano mzuri wan chi yetu.

 

Hata Mweyeki Sleiman ameitaka Wizara hiyo kuweza kuzisimamia ipasavyo nyumba kwa kua katika hadhi zinazoendana na viongozi pamoja na kuhakikisha mradi huo unamilizika kwa wakati uliopangwa.

“hakikisheni mnasimami vyema mradi wa nyumba za viongozi kwa kuona kuwa zinamalizika katika uliopangwa alisisitza”

 

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi kwa KIPINDI cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022, kwa Wizra yake,Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Riziki Pembe Juma, alisema kuwa jumla ya shilingi Bilioni 11.919 zimepangwa kutumika ambapo jumla ya shilingi Bilioni 10.310 ni fedha za maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za viongozi na Bilioni 1.609 kwa kazi za kawaida.

Alisema hadi kufikia Septemba 2021 jumla ya shilingi milioni 91.950 zimeshatumika kwa kazi za kawaida sawa na asilimia 32 ya makadirio na hakuna fedha iliyotumika kwa kazi za maendeleo kutokana na yaliyojitokeza ya mradi mzima.

 

Akilitolea ufafanuzi Shirika la Nyumba la Zanzibar Waziri Pembe alifahamisha kuwa, Shirika lilipangiwa kukusanya jumla ya shilingi 780.000 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato hadi kufikia September 2021 Shirika limekusanya jumla ya shilingi Bilioni 2.269 sawa na wastani wa asilimia 291 ya makadirio ya makusanyo hayo.

 

 

 

 

Mhe. Riziki amewataka wapangaji wanaosihi katika nyumba za Shirika kuhakikisha kuwa Nyumba hizo wanazitumia kwa matumizi sahihi pamoja na kuhamiska Zaidi katika ulipaji kodi ili kuliwzesha Shirika hilo kuweza kupiga hatua Zaidi kimaendeleo kwa maslahi ya nchi yetu.

 

Alifahamisha kuwa mbali na changamoto zinazolikabili shirika hilo lakini shirika limekuwa likichukua juhudi za mara kwa mara katika kuhakikisha wapangaji wake wanalipa kodi kwa wakati pamoja na kuwahamasisha wapangaji hao kuzitunza na kuzitumia nyumba kwa matumizi sahihi.

 

‘’Shirika la nyumba limekuwa likichua jitihada ya kuelimisha jamii kupitia vyomba vya habari kuhusiana na ulipakaji kodi kwa wakati jambo ambalo liepelekea kupiga hatua katika ukusanyaji wa mapato yake kwa kipindi hiki”alisisitiza”

Aidha Mhe. Riziki amewataka wapangaji wanaosihi katika nyumba za Shirika kuhakikisha kuwa Nyumba hizo wanazitumia kwa matumizi sahihi pamoja na kuhamiska Zaidi katika ulipaji kodi ili kuliwzesha Shirika hilo kuweza kupiga hatua Zaidi kimaendeleo kwa maslahi ya nchi yetu.

 

‘’niwaombe wapangaji wanaoishi katika nyumba za shirika kuhakikisha tunazitumia vyema nyumba hizi kwa kuzitunza na kuziweka katika mandhari nzuri pamoja na kuendelea kulipa kodi kwa wakati”alisema’’

Hata hivyo aliishauri Kamati hiyo kuendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na Wizara yake ili kutekeleza programu mbali mbali zilizopangwa na ofisi hiyo kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

 

Aidha aliipongeeza Kamati hiyo kwa maelekezo na ushauri ilioutoa na kuahidi kuwa itaufanyia kazi kwa lengo la kuongeza ufanisi na mapato ya serikali.

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wajumbe wa kamati hiyo, mkurugenzi wa shirika la nyumba, mwanaisha ali said, alieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na jitihada pamoja na mashirikiano mazuri baina ya Uongozi mzima wa Wizara ya Ardhi na Watendaji wa Shirika hilo katika kuona kuwa Shirika lizidi kuimarika kiuendaji.

 

Aliongeza kuwa licha ya changamoto hiyo, shirika linaendelea na ukarabati wa jumba namba moja katika nyumba za maendeleo michezani,jumba la mnadani Darajani kwa Unguja na jumba namba moja Madungu kwa Pemba.

Amefahamisha ukarabati wa nyumba za maendelea unaendelea hatua baada ya hatua hadi kuweza kuyamalizia majumba yote na kuufanya mji wetu uwe katika muonekano mzuri.

“kadri hali ya fedha itakaporuhsu tutaendelea kuyafanyia ukarabati majumba yote kwani lengo la Shirka ni kuhakikisha inatimiza majukumu yake kwa vitendo kwa kuwawekea wapangaji wake mandhari nzuri na salama”alisisitiza”

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Joseph John Kilangi, alieleza kuwa pamoja na kusimamia uendeshaji wa shirika la nyumba na taasisi nyengine zilizomo ndani yake Wizara imeshakamilisha master plan ya mji mpya wa kilimani ambapo unatarajiwa kujengwa mara baada ya taratibu zote za kiutendaji kumalizika.

 

Katibu Mkuu Mhe.Joseph John Kilangi, alieleza kuwa pamoja na kusimamia uendeshaji wa shirika la nyumba na taasisi nyengine zilizomo ndani yake Wizara imeshakamilisha master plan ya mji mpya wa kilimani ambapo unatarajiwa kujengwa mara baada ya taratibu zote za kiutendaji kumalizika.

 

“tunatarajia kujenga mji mpya wa kilimani amabao utatoa haiba na muonekano mzuri wa mji wetu mara tu taratibu za kiutendaji kumalziika”alifahamisha

Aidha Katibu Mkuu huyo alifahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepata bahati ya kushirika maonesho ya Export Dubai ambapo kwa Tanzania inategemewa kushiriki mwezi wa Februari 2022.

 

Amefahamisha kuwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi nayo imepata bahati ya kushiriki maonesho hayo hasa katika sekta ya ujenzi na kuweza kuzitangaza fursa mbalimbali za ujenzi wa mji mpya.

 

“Katika ushiriki wa Maonesho hayo tutaweza kupata nafasi ya kuzitangaza fursa mbalimbali zilizomo ndani ya sekta ya ujenzi na kuweza kufikia malengo ya mipango miji”alisema.

 

Nao wajumbe hao wameitaka Wizara hiyo kuweza kuzifanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza ili kuweza kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya awamu ya nane

inayoongozwa Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyeiki wa Baraza la Mapinduzi katika kuleta maendeleo kwa wote.