MHE RIZIKI PEMBE JUMA AKIFUNGUA MASHINDANO YA MCHEZO WA SQUASH

MHE RIZIKI PEMBE JUMA  AKIFUNGUA MASHINDANO YA MCHEZO WA SQUASH

 

Chama cha Mpira wa Ukuta Zanzibar Squash Courts kimetakiwa kutumia mbinu bora za kushindana kwa lengo la kupata wacheza bora watakaorozeshwa katika Shirikisho la Mpira wa Ukuta la Afrika(Squash Federation of Afrika.)

Mhe.Waziri amekitaka chama hicho pia kutumia wataalamu wenye sifa ambao wataweza kufundisha vijana wetu ili kuweza kupata wachezaji watakaokidhi viwango vya kimataifa na kuweza kushinda katika mashindano ya kikanda na kimatifa na kuiletea sifa nchi yetu.

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe Riziki Pembe Juma amesema hayo huko maisara wakati alipokua akifungua mashindano ya mchezo wa Squash kwa lengo la kuona mchezo huo unakua kimataifa.

Aidha Mhe.Waziri amekitaka chama hicho pia kutumia wataalamu wenye sifa ambao wataweza kufundisha vijana wetu ili kuweza kupata wachezaji watakaokidhi viwango vya kimataifa na kuweza kushinda katika mashindanoya kikanda na kimatifa na kuiletea sifa nchi yetu.

Mapema akimkaribisha Waziri Wa Ardhi,Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Fatma Hamad Rajabu amefahamisha kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ni kuhakikisha inaendeleza michezo kwa Vitendo.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Vijana na Michezo Bi.Fatma Hamad Rajabu amefahamisha kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ni kuhakikisha inaendeleza michezo kwa Vitendo.

Hivyo Katibu Mkuu amewahakikishia wanamichezo hao kuwa Wizara yake itakua nao bega katika kuihamisisha jamii na kuona kwamba mchezo huo unaendelea kukua na kuleta faida kwa kutoa ajira kwa vijana.

Wakielezea changamoto zinazowakabili katika chama chao mmoja ya wanamichezo wa mchezo huo Mohamed Hamza emesema kuwa chama cha mpira wa Ukuta Zanzibar Squash Fitness Club kinakabiliwa na tatizo la vitendea kazi pamoja ufadhili wa kuweza kukisaidiia chama hicho kufikia malengo yake hivyo wameiomba Wizara ya Habari  Sanaa na Michezo kuweza kuwaangalia kwa jicho la huruma.

 

Mohamed Hamza emesema kuwa chama cha mpira wa Ukuta Zanzibar Squash Fitness Club kinakabiliwa na tatizo la vitendea kazi pamoja ufadhili wa kuweza kukisaidiia chama hicho kufikia malengo yake hivyo wameiomba Wizara ya Habari Sanaa na Michezo kuweza kuwaangalia kwa jicho la huruma.

Sambamba na hayo Mhe.Waziri pia alipata nafasi ya kushuhudia mechi ndogo iliyoaandaliwa na chama hicho ambapo Saleh juma aliweza kuibuka kidedea kumshinda mpizani wake Mohammed Hamza kwa seti Tatu kwa Moja.