TAARIFA KWA UMMA
17 Nov 2021

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Wizara wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imesema kuwa Azma ya Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ni kuhakikisha  inayapanga Maeneo yote ya Mikoa Unguja na Pemba ili kuepusha ujenzi holela.

 

Mhe.Riziki Pembe Juma akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokuwa akitoa taarifa  ya utekeleza kwa Wizara yake katika ofisi za Wizara hiyo Maisara Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Riziki Pembe Juma amesema kuwa kufanya hivyo kutaweza kuweka haiba nzuri ya maeneo pamoja na kupanga matumizi yanayozingatia uwiyano wa idadi ya watu mijini na vijijini. 

Akielezea mipango mbalimbali kwa Wizara yake hasa katika sekta ya Ardhi Mhe.Waziri amesema kuwa Wizara yake inatekeleza Mipango mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wake mipango hiyo ikiwa ni pamoja na utambuzi na usajili wa ardhi, upangaji na upimaji  wa maeneo ya makaazi na uwekezaji pamoja na ujenzi wa nyumba za viongozi.

Aidha Mhe Riziki amesema kuwa Wizara katika kuyafikia malengo yake hasa katika sekta ya Ardhi Wizara   imeanza kushirikiana na kampuni binafsi kuyapima na kuyapanga upya maeneo mbalimbali ya uwekezaji na maakazi yakiwemo maeneo maalum ya uwekezaji wa viwanda (indusrial park)dunga,pangatupu na chamanangwe.

Hata hivyo Mhe. Riziki amesema kuwa katika kuimarisha Sekta ya Makaazi Wizara inaendelea na juhudi ya kuziboresha nyumba za maendeleo pamoja na kutafuta makampuni na wadau ili kuwekeza katika sekta ya nyumba.

‘’mchakato wa ujenzi wa nyumba za maendeleo unaendelea kwa kushirikiana na sekta binafsi katika maeneo mbalimbali ya     Unguja na Pemba’’ alisisitiza.

Kwa upande wa usimamizi na matumizi bora ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi unaozingatia sheria,sera na miongozo Mhe Riziki amefahamisha kuwa Wizara inahakikisha kunakuwepo na matumizi bora na endelevu ya Ardhi,usajili wa Ardhi pamoja na utatuzi wa migogoro.

‘’ Wizara inahakikisha inasimamia kwa kila hatua suala la  utambuzi na upatikanaji wa hati za haki ya matumzi ya Ardhi na makaazi yaliyo salama na nafuu kwa wananchi wote wa Zanzibar‘’ alisema’’

Akizungumzia kuhusiana na jitihada za uimarishaji mapato na kuzingatia mchango wa sekta ya Ardhi kwa Maendeleo ya uchumi na jamii Mhe.Riziki amefahamisha kuwa Wizara imefanya uhakiki wa maeneo ya uwekezaji na kubaini uwepo wa changamoto kadhaa katika maeneo hayo ikiwemo maeneo mengi hayajaendelezwa na baadhi yao hawana Mikataba ya ardhi.

 ‘’ katika uhakiki uliofanyika Wizara pia imegundua kuna baadhi ya wanatumia hati za haki ya matumizi ya ardhi(CRO)katika maeneo ya uwekezaji ambapo ni kunyume na sheria ilioyowekwa’’ alisisitiza‘’

Kupitia changamoto hizo Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi inatoa indhari kuwa wawekezaji wote wa kigeni ambao hawajaendeleza maeneo yao na wanayo Mikataba ya Ukodishwaji ardhi(Land Lease Agreement)wanatakiwa kuendeleza maeneo yao kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

Aidha Wizara pia inawataka wananchi na wawekezaji wazalendo(wazawa)kuyaendeleza maeneo yao kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe ya tarifa hii ikiwa hakutakuwa na uendelezaji maeneo hayo yatafutwa na kurudi Serikalini.

Hata hivyo Mhe.Riziki amewataka wawekezaji na wananchi ambao ardhi wananzozitumia kwa uwekezaji na wana hati za haki ya matumizi ya Ardhi kwa Makaazi (CRO)kufika Wizarani na kuomba Mikataba ya ukodishwaji ardhi(land lease agreement)ili ktumika kwa uwekezaji na sio makaazi kama ilivyo sasa.

Mkutano huo wa utoaji taarifa ya utekelezaji wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kwa waandishi wa Habari kufuatia Agizo la Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kuzitaka kila Taasisi za Serikali  kuelezea utekelezaji na Mikakati ya Wizara yake kwa lengo la kuongeza ufanisi.