Mhe. Rahma Kassim Ali
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
Karibu Wizara ya Ardhi
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imeanzishwa kwa tangazo la kisheria Nam: 137 ya mwaka 2020 na Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi na kuainisha majukumu ya wizara na taasisi zitakazoundwa katika kusimamia Ardhi na Makaazi bora kwa jamii.
DIRA
Kuwa muhimili wa uhakika na wa usalama wa umiliki na matumizi ya Ardhi na Makaazi endelevu kwa maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.
Dhamira
Kuhakikisha kwamba Ardhi ya Zanzibar inatoa mchango mkubwa kwa ustawi wa Taifa kupitia mipango bora ya matumizi ya Ardhi kwa ajili ya huduma za makaazi na kiuchumi